Mapasta na mafusaki wanaosilimu na papohapo wanakuwa walinganizi

Swali: Leo ni jambo lililoenea wale wenye kutubia madhambi makubwa yenye kujulikana papohapo wanakuwa ni walinganizi na wanaandaliwa ili wawe walinganizi. Wanatumia hoja kwa wale wachawi wa Fir´awn ya kwamba waliposilimu na wakatubia walifika papohapo wanakuwa ni walinganizi na wanachuoni…

Jibu: Ni vipi walikuwa walinganizi na wanachuoni papohapo? Waliuawa papohapo na wakasulubiwa. Hawakuwa hayo. Ni kweli kuwa walitubia. Lakini ametoa wapi kusema kwamba walikuwa walinganizi na wanachuoni?

Da´wah inahitajia elimu. Sio mtu kuingia pale tu anapotubia. Isipokuwa ikiwa kama kabla ya hapo aliuwa ni mwanachuoni na alikuwa na elimu kisha akatubia kwa Allaah. Katika hali hii alinganie katika dini ya Allaah kutokana na ile elimu alionayo. Lakini iwapo alikuwa ni mjinga kisha akatubia anahitajia kwanza ajifunze.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (16) http://alfawzan.af.org.sa/node/2059
  • Imechapishwa: 01/05/2017