Swali: Wanazuoni wametofautiana kuhusu kuchenguka kwa wudhuu´ wa mtu anayegusa dhakari yake. Wanaosema kwamba wudhuu´ wake haubatiliki wametolea dalili Hadiyth isemayo:
“Hiyo si chochote isipokuwa sehemu ya mwili wako.”
Ni maoni yepi yenye nguvu zaidi?
Jibu: Maoni yenye nguvu zaidi miongoni mwa maono za wanazuoni katika suala hili ni maoni ya wanazuoni wengi, kwamba wudhuu´ wa mwenye kugusa dhakari yake unabatilika. Hii ni kwa sababu Hadiyth isemayo:
“Hiyo si chochote isipokuwa sehemu ya mwili wako”
ni dhaifu. Haiwezi kupingana na Hadiyth Swahiyh zinazofahamisha kwamba mwenye kugusa dhakari yake anatakiwa kutawadha. Msingi ni kwamba amri inajulisha uwajibu. Hata tukikadiria kwamba Hadiyth hiyo si dhaifu, basi imefutwa hukumu yake na Hadiyth isemayo:
“Yule mwenye kugusa dhakari yake, basi atawadhe.”
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/263-264)
- Imechapishwa: 11/11/2026
Swali: Wanazuoni wametofautiana kuhusu kuchenguka kwa wudhuu´ wa mtu anayegusa dhakari yake. Wanaosema kwamba wudhuu´ wake haubatiliki wametolea dalili Hadiyth isemayo:
“Hiyo si chochote isipokuwa sehemu ya mwili wako.”
Ni maoni yepi yenye nguvu zaidi?
Jibu: Maoni yenye nguvu zaidi miongoni mwa maono za wanazuoni katika suala hili ni maoni ya wanazuoni wengi, kwamba wudhuu´ wa mwenye kugusa dhakari yake unabatilika. Hii ni kwa sababu Hadiyth isemayo:
“Hiyo si chochote isipokuwa sehemu ya mwili wako”
ni dhaifu. Haiwezi kupingana na Hadiyth Swahiyh zinazofahamisha kwamba mwenye kugusa dhakari yake anatakiwa kutawadha. Msingi ni kwamba amri inajulisha uwajibu. Hata tukikadiria kwamba Hadiyth hiyo si dhaifu, basi imefutwa hukumu yake na Hadiyth isemayo:
“Yule mwenye kugusa dhakari yake, basi atawadhe.”
Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/263-264)
Imechapishwa: 11/11/2026
https://firqatunnajia.com/maoni-ya-wanazuoni-wengi-kuhusu-anayegusa-tupu-yake-baada-ya-kutawadha/