Swali: Ni mambo gani yanayopendekezwa kufanywa wakati wa kutawadha?
Jibu: Namna ya wudhuu´ iliyowekwa katika Shari´ah ni kwamba mtu amimine maji kutoka kwenye chombo juu ya viganja vyake mara tatu, kisha aingize mkono wake wa kulia ndani ya chombo, asukutue na kupandisha maji puani mara tatu. Kisha aoshe uso wake mara tatu, aoshe mikono yake mpaka kwenye viwiko mara tatu, kisha apanguse kichwa chake na masikio yake mara moja, halafu aoshe miguu yake mpaka kwenye vifundo vya miguu mara tatu. Inasihi ikiwa ataosha viungo hivyo mara mbilimbili au mara mojamoja. Baada ya wudhuu´ aseme:
أشهد ألا إله إلا الله وحده لا شريك له وأشهد أن محمدا عبده ورسوله اللهم اجعلني من التوابين واجعلني من المتطهرين
“Nashuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake. Ee Allaah! Nijaalie niwe miongoni mwa wanaotubia na nijaalie niwe miongoni mwa wanaojitakasa.”
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/231)
- Imechapishwa: 11/11/2026
Swali: Ni mambo gani yanayopendekezwa kufanywa wakati wa kutawadha?
Jibu: Namna ya wudhuu´ iliyowekwa katika Shari´ah ni kwamba mtu amimine maji kutoka kwenye chombo juu ya viganja vyake mara tatu, kisha aingize mkono wake wa kulia ndani ya chombo, asukutue na kupandisha maji puani mara tatu. Kisha aoshe uso wake mara tatu, aoshe mikono yake mpaka kwenye viwiko mara tatu, kisha apanguse kichwa chake na masikio yake mara moja, halafu aoshe miguu yake mpaka kwenye vifundo vya miguu mara tatu. Inasihi ikiwa ataosha viungo hivyo mara mbilimbili au mara mojamoja. Baada ya wudhuu´ aseme:
أشهد ألا إله إلا الله وحده لا شريك له وأشهد أن محمدا عبده ورسوله اللهم اجعلني من التوابين واجعلني من المتطهرين
“Nashuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake. Ee Allaah! Nijaalie niwe miongoni mwa wanaotubia na nijaalie niwe miongoni mwa wanaojitakasa.”
Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/231)
Imechapishwa: 11/11/2026
https://firqatunnajia.com/ni-mambo-gani-yanayopendekezwa-kufanywa-wakati-wa-kutawadha/