Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

183 – Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

بَايَعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم عَلَى إقَامِ الصَّلاةِ، وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ، والنُّصْحِ لِكُلِّ مُسْلِمٍ

“Nilimpa ahadi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kusimamisha swalah, kutoa zakaa na kumnasihi kila muislamu.”[1]

Katika kusimamisha swalah kwa nisba ya wanaume ni pamoja vilevile na kuswali kwa mkusanyiko katika misikiti. Hili pia ni katika kusimamisha swalah. Mwenye kuacha swalah bila ya udhuru anapata dhambi. Bali mpaka baadhi ya wanachuoni wamefikia kuonelea kuwa akiacha kuswali na mkusanyiko bila ya udhuru, swaalah yake ni batili na anarudishiwa mwenyewe. Haikubaliwi. Lakini kauli ya wanachuoni wengi – na ndio kauli sahihi zaidi – wanaonelea kuwa swalah yake ni sahihi pamoja na kuwa anapata dhambi. Hii ndio kauli yenye nguvu na yenye kujulikana kwa Hanaabilah na ndio kauli ya wanachuoni wengi wale ambao wanaonelea kuwa swalah ya mkusanyiko ni wajibu.

[1]al-Bukhaariy (57) na Muslim (56).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/399-400)
  • Imechapishwa: 30/07/2025