Imaam at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Watu wa Peponi kumuona Allaah ni haki pasi na kumzunguka wala namna.”

Kumuona Allaah kabla ya kuingia Peponi wanachuoni wana kauli tatu:

1 – Waumini watamuona Mola Wao kwenye kiwanja kabla ya kuingia Peponi. Hakuna wataomuona isipokuwa waumini peke yao.

2 – Waumini na makafiri wote wawili watamuona katika kiwanga kisha baada ya hapo atajizuia makafiri hawatomuona tena.

3 – Waumini na wanafiki watamuona. Hayo yamethibiti katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy na Muslim.

Hizi ni kauli tatu za wanachuoni. Kuhusiana na waumini kumuona Mola wao Peponi, hili ni suala lisilokuwa na shaka yoyote. Masuala kuhusiana na waumini kumuona Mola wao Peponi ni katika mambo matukufu kabisa miongoni mwa mambo ya misingi ya dini. Mambo haya kwa ajili yake wameshindana wenye kushindana na kwa ajili yake kuna ambao wamezuiwa kumuona Mola Wao.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/216)
  • Imechapishwa: 30/05/2020