Manii yanayotoka baada ya kuoga josho la janaba

Swali: Je, ni lazima kwangu kurudia kuoga ikiwa nitaoga josho la janaba na nikamaliza kisha nikatokwa na kitu katika manii?

Jibu: Haikulazimu kurudia kutawadha muda wa kuwa umekwishaoga. Manii haya hayana maana yoyote kwa sababu yametoka pasi na matamanio. Hukumu yake ni kama mkojo unaowajibisha kujisafisha na maji na kutawadha. Josho la lazima umekwishalitekeleza. Vivyo hivyo mtu akishaoga kisha baada ya hapo akatokwa na manii, basi manii hayo ni kama mkojo ambao haulazimishi kuoga muda wa kuwa unatokana na jimaa iliotangulia. Lakini kama yametoka kutokana na shahawa mpya iliyompata kwa sababu ya kugusagusa, kubusu au sababu nyingine ya kuamsha matamanio, basi hayo ni manii mepya yanayowajibisha kuoga.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/188)
  • Imechapishwa: 28/08/2021