Maneno yenye mpangilio wa vina katika Khutbah na du´aa

Swali: Je, inajuzu kutumia maneno yenye mpangilio wa vina (السجع) katika Khutbah na katika du´aa?

Jibu: Kutumia mtindo huo katika Khutbah hakuna neno ikiwa haisababishi mashaka wala haisumbui wasikilizaji. Iwapo ni mpangilio mwepesi ambao hautungwi kwa makusudi, bali inatoka kiasili kwenye ulimi bila juhudi ya kuibuni, hakuna ubaya ndani yake. Lakini ikiwa inatungwa kwa makusudi na mtu anajilazimisha kuiunda, haifai kufanya hivyo. Hali yake ya chini ni kuwa inachukiza, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimlaumu aliyefanya hivyo na akausifu kama ni ushairi wa makuhani[1]. Kwa hivyo mpangilio wa ushauri usiyotungwa makusudi, bali unatoka kiasili kwa mtu bila kujilazimisha, haina tatizo. Tofauti na ile ya kubuni na kujitafutia maneno, ambayo mara nyingi huwafanya wasikilizaji wafedheheke nayo, inaweza kuzaa sentensi zisizo na haja au zisizo na faida, na wakati mwingine pengine ukawa na madhara pasi na faida. Pia ndani yake kuna kujifananisha na makuhani kwa mpangilio wao za kuchanganya haki na batili.

[1] al-Bukhaariy (5758) na Muslim (1681).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1088/هل-يجوز-السجع-في-الخطب
  • Imechapishwa: 24/01/2026