Maneno ya mwisho kusema kabla ya kulala

Swali: Kunabaguliwa kusema ”Laa ilaaha illa Allaah” ile Dhikr wakati wa kulala cha mwisho anachotakiwa mtu kusema:

اللهم أسلمت نفسي إليك و وجهت وجهي إليك و فوّضتُ أمري إليك و ألجأتُ ظهري إليك رغبةً و رهبةً إليك لا ملجأ و لا منجا منك إلا إليك. آمنت بكتابك الذي أنزلت و بنبيك الذي أرسلت

“Ee Allaah! Nimeisalimisha nafsi yangu Kwako. Nimeuelekeza uso wangu Kwako. Nimekuachia mambo yangu Wewe. Nimeutegemeza mgongo wangu Kwako. Nafanya hivyo kwa matarajio na kwa kukuogopa. Hapana sehemu ya kukimbilia wala ya kujiokoa ila Kwako. Nimekiamini kitabu Chako ulichokiteremsha na Mtume Wako Uliyemtuma.”?

Jibu: Hayo ni wakati wa kufa. Hayo yamepokelewa katika Hadiyth wakati wa kifo. Hili ni maalum na hilo jengine ni lenye kuenea. Hilo jengine linapendeza kukithiri kusema hivo wakati wa maradhi na khaswa wakati kumedhihiri alama za kifo ili maneno yake ya mwisho kusema yawe ni ”Laa ilaaha illa Allaah”. Hili jengine ni wakati wa kulala maneno yake ya mwisho kusema iwe:

اللهم أسلمت نفسي إليك

“Ee Allaah! Nimeisalimisha nafsi yangu Kwako… ”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23963/معنى-من-كان-اخر-كلامه-لا-اله-الا-الله
  • Imechapishwa: 08/08/2024