Mambo ya romantiki na mwenye hedhi

Swali: Je, ni bora kuepuka kuchanganyika na mwanamke mwenye hedhi?

Jibu: Hakuna tatizo kuchanganyika naye. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akifanya hivo. Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akilala naye.

Swali: Ni kana kwamba msingi ni kuepuka?

Jibu: Hayo ni kuhusu ile sehemu iliyo chini ya nguo yake ya chini. Epuka sehemu iliyo chini ya nguo yake ya chini. Kwa msemo mwingine alale naye na avae kikoi au suruwali na asiwe uchi kabisa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24767/حكم-مباشرة-الحاىض
  • Imechapishwa: 12/12/2024