Mambo ya kukusaidia kudumu na kisimamo cha usiku

Swali: Vipi nitahifadhi kuswali daima kisimamo cha usiku?

Jibu: Kitu cha kwanza ni nia. Utaponuia hili na ukaliazimia kwa moyo wako, hili litakusaidia kusimama usiku na mwishowe utazowea.

Pili kulala mapema. Lala mwanzoni mwa usiku ili upate kuamka mwisho wa usiku.

Tatu weka kengele [alamu] ya kukuamsha. Itapofika wakati unaotaka kuamka itakuzindua kuamka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (38) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-2-4_1.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020