Swali: Je, ni haramu kwa mwanamke kukaa chemba na mume wa msichana wake?

Jibu: Mume wa msichana wake ni Mahram yake. Baadhi ya wanawake wana aibu sana. Bora ni yeye asijisitiri mbele yake na afanyie kazi ruhusa  ya Allaah:

“Hakika Allaah anapenda ifanyiwe kazi ruhusa Yake.”

Hiyo inakuwa ni aibu kwa mwanamke kujizuilia na wanaume wasioweza kumuoa. Hata hivyo ikiwa kuna sababu nyenginezo kwa mfano ni mwanaume asiyeaminika na kwamba anafanya mambo kadhaa yasiyokuwa ya sawa, basi anaweza kujizuilia muda wa kuwa yuko na sababu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23922/ما-حكم-خلوة-المراة-بزوج-ابنتها
  • Imechapishwa: 01/06/2024