Swali: Mimi ni mwanamke nina wasichana wanane ambapo wanne wameshaolewa. Wawili ninajisitiri mbele ya waume zao na wengine wawili nawafunulia Hijaab waume zao. Naomba mnifafanulie, je, nina kosa katika hilo? Je, Hijaab kwao inajuzu?
Jibu: Waume wa wasichana zako ni Mahram kwako. Kwa hivyo hakuna ubaya kuwafunulia yale yaliyozoeleka, kama uso, mikono na miguu. Hilo si wajibu. Lakini ndilo lililopendekezwa Kishari´ah. Hilo ni kutokana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Chukueni ruhusa ya Allaah aliyokuruhusuni.”[1]
”Hakika Allaah anapenda ruhusa Zake zitumiwe.”[2]
Kwa sababu kujisitiri mbele yao ni kinyume na Shari´ah na kunasababisha ugeni na chuki. Kwa hiyo linalopaswa ni kuacha hilo na kufanya kwa mujibu wa ruhusa ya Kishari´ah. Kuwafunulia baadhi yao na kuwaficha wengine kunasababisha shaka na maswali, na pia kunasababisha ugeni na kutoelewana. Kwa hivyo linalopendekezwa ni kuacha kufanya hivyo, ama kuwafunulia wote au kuwazuia wote kwa njia inayofanana.
[1] Muslim (1115).
[2] Ahmad (2/108) na Ibn Hibbaan (2742).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/26)
- Imechapishwa: 18/03/2026
Swali: Mimi ni mwanamke nina wasichana wanane ambapo wanne wameshaolewa. Wawili ninajisitiri mbele ya waume zao na wengine wawili nawafunulia Hijaab waume zao. Naomba mnifafanulie, je, nina kosa katika hilo? Je, Hijaab kwao inajuzu?
Jibu: Waume wa wasichana zako ni Mahram kwako. Kwa hivyo hakuna ubaya kuwafunulia yale yaliyozoeleka, kama uso, mikono na miguu. Hilo si wajibu. Lakini ndilo lililopendekezwa Kishari´ah. Hilo ni kutokana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Chukueni ruhusa ya Allaah aliyokuruhusuni.”[1]
”Hakika Allaah anapenda ruhusa Zake zitumiwe.”[2]
Kwa sababu kujisitiri mbele yao ni kinyume na Shari´ah na kunasababisha ugeni na chuki. Kwa hiyo linalopaswa ni kuacha hilo na kufanya kwa mujibu wa ruhusa ya Kishari´ah. Kuwafunulia baadhi yao na kuwaficha wengine kunasababisha shaka na maswali, na pia kunasababisha ugeni na kutoelewana. Kwa hivyo linalopendekezwa ni kuacha kufanya hivyo, ama kuwafunulia wote au kuwazuia wote kwa njia inayofanana.
[1] Muslim (1115).
[2] Ahmad (2/108) na Ibn Hibbaan (2742).
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/26)
Imechapishwa: 18/03/2026
https://firqatunnajia.com/mama-mkwe-anajisitiri-mbele-ya-wakwe-zake/