Mama hataki watoto wende katika darsa za wanachuoni

Swali: Mimi na ndugu tunaenda katika darsa za wanachuoni. Siku moja mamangu alimkasirikia kaka yangu na akatukataza kwenda katika darsa za wanachuoni. Je, ni lazima kumtii?

Jibu: Hapana. Asiwakatazeni kwenda katika darsa za wanachuoni wala kutafuta elimu. Jaribu kumkinaisha na kuweni wazuri kwake. Akiendelea kung´ang´ania msikubali maneno yake. Nendeni kwenye darsa za wanachuoni.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (40) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighatsah%20%20-%2028%20-%2012%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017