Swali: Allaah amesema:

مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ

“Hatamki yeyote neno isipokuwa anaye mchungaji aliyejitayarisha kuandika.”[1]

Hii ina maana kwamba Malaika wanaandika kila kitu?

Jibu: Ndio, wanaandika kila kitu. Lakini atawajibishwa kwa yale yenye kheri na shari. Ikiwa ni ya kheri analipwa thawabu kwayo na ikiwa ni ya shari anapata dhambi kwayo. Yasiyokuwa hayo kinaachwa.

[1] 50:18

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/2775/476-من-كتاب-الامور-المنهي-عنها
  • Imechapishwa: 07/11/2024