Swali: Hadiyth inayosema kwamba Ummah huu utagawanyika katika makundi sabini na tatu ina maana kwamba watadumishwa Motoni milele?

Jibu: Inavyotambulika ni kwamba hawa ni wazushi. Wamepewa makemeo ya Moto. Kwa sababu wanachuoni wamesema kuwa Jahmiyyah, Suufiyyah, Raafidhwah na Qadariyyah waliopindukia ni wenye kutoka katika makundi haya sabini na tatu. Hawa ni makafiri. Ni dalili inayothibitisha kuwa makundi haya sabini na tatu ni wazushi. Wamepewa matishio ya Moto kama watenda madhambi makubwa wengine.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (04) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/431/431.mp3
  • Imechapishwa: 07/08/2018