Makosa kufanya masomo baada ya ´Aswr siku ya ijumaa?

Swali: Baadhi ya watu wasiokuwa na elimu wanamkemea ambaye anawasomea waumini baada ya swalah ya ´Aswr siku ya ijumaa. Je, kumepokelewa chochote juu ya hilo?

Jibu: Hapana, hakuna makatazo kabla ya swalah ya ijumaa. Ama baada ya swalah tulikuwa tukisoma. Na hivi sasa haya ni masomo tunayofanya baada ya swalah ya ´Aswr siku ya ijumaa. Makatazo ni kabla ya swalah ya Fajr na kufanya mviringo wa kielimu kabla ya swalah ya ijumaa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (17)
  • Imechapishwa: 14/11/2020