Makemeo makali kwa ambao hawaoshi vyema visigino vyao

Swali: Ni maana ya maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Ole visigino kutokana na Moto.”[1]?

Jibu: Maana yake ni ulazima wa kuosha visigino na kuvipa umuhimu wakati wa kutawadha. Aoshe vifundo viwili vya miguu. Asichukulie jambo hili kwa uzito mdogo, kwa sababu vifundo viwili ni miongoni mwa sehemu zinazopaswa kuoshwa. Vilevile viwiko viwili vya mikono. Viwiko huoshwa pamoja na mkono, na vifundo huoshwa pamoja na miguu. Inawajibika kuosha vifundo na viwiko, kwani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anatawadha alikuwa akiosha mikono yake na alikuwa akianza juu hadi kwenye bega. Aidha anapoosha miguu yake alikuwa akianza juu hadi kwenye muundi. Kwa maana nyingine anaosha vifundo na viwiko kikamilifu.

[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (219).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31702/ما-معنى-حديث-ويل-للاعقاب-من-النار
  • Imechapishwa: 16/11/2025