Jumuiya ya al-Hikmah imejengeka juu ya uwongo na ulaghai kuanzia siku ya kwanza. Uwongo gani? Wanawaeleza watu huko Adeni – hata kwenye barua iliotumwa kutoka Makka – kwamba mimi niko naridhia jambo hilo. Mimi nakaripia mambo ya uvyamavyama kuanzia siku ya kwanza. Ulaghai gani? Wanawalaghai watu eti sisi tunakataza kujengwa kwa misikiti, kuwatunza mayatima, kuchimba visima na mambo mengine yenye manufaa yanayokubaliwa na dini. Ikiwa jumuiya bora kabisa ya Yemen imejengwa juu ya uwongo na ulaghai huu, una unasemaje kuhusu mataasisi mengine? Mimi naona kuwa yeyote anayesaidia jumuiya hizi anapata dhambi, kwa sababu mtu ataulizwa juu ya mali yake. Abu Barzah al-Aslamiy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
“Haitovuka miguu ya mja siku ya Qiyaamah mpaka aulizwe juu ya mambo mane: umri wake aliuteketeza katika mambo gani, elimu yake aliifanyia nini, mali yake aliipata kivipi na akaitumia wapi na mwili wake aliutumia vipi?”[1]
Namna hii ndivo wanavofanya al-Ikhwaan al-Muslimuun kcuheza na akili za vijana. Wanawaweka mbali na kuhifadhi Qur-aan na kwenda kuigiliza, kuimba Anaashiyd na kuchukia Sunnah na Ahl-us-Sunnah. Wewe unatoa pesa zako kwa ajili ya Allaah, lakini wao wanazitumia kwa ajili ya kusaidia na kukitia nguvu kipote chao. Mimi sijuzishi mfano wa jumuiya hizi. Jitenge mbali na mapote mengine yote ambali dogo liwezalo kusemwa juu yake ni kwamba yamezuliwa.
[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (1/162).
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 191-192
- Imechapishwa: 03/08/2025

Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 191-192
Imechapishwa: 03/08/2025
https://firqatunnajia.com/makatazo-ya-kuwapa-michango-hizbiyyuun/