Makatazo ya kuwanyamazia ISIS

Swali: Vijana kadhaa katika nchi yangu ya Amerika Kusini wamejiunga na ISIS kwa hoja kwamba ukhaliyfah ni wa haki. Sasa wanawashauri vijana wengine kufanya vivyo hivyo. Unawashauri nini?

Jibu: Ni lazima mbainishe. Wabainishieni watu wa nchini mwenu. Wabainishieni na wawekeeni wazi ´Aqiydah ya kundi hili kwa wale wanaokubali nasaha. Huo ndio wajibu wenu. Msinyamaze ilihali mnao uwezo wa kuweza kubainisha na kuweka wazi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
  • Imechapishwa: 05/07/2024