Swali: Inasemwa kwamba imamu hubeba baadhi ya wajibu kwa niaba ya maamuma. Tunaomba ufafanuzi wa hilo na bayana ya mambo anayobeba.
Jibu: Ndiyo, imamu hubeba baadhi ya mambo kwa niaba ya maamuma. Miongoni mwa hayo ni kwamba yeye hubeba jukumu la sijda ya kusahau kwa niaba yao. Ikiwa maamuma atasahau, basi yeye habebeshwi kitu. Bali imamu ndiye atasujudu nao maamuma husujudu pamoja naye. Ama sahau ya maamuma peke yake wakati yuko nyuma ya imamu, haiwezi kumdhuru. Hairuhusiwi kwake kufanya sujuud ya kusahau peke yake ikiwa ameanza swalah pamoja na imamu tangu mwanzo. Katika hali hiyo imamu hubeba hilo kwa niaba yao. Mfano ni pale imamu anapoacha Tashahhud ya kwanza kwa kusahau na kusimama, basi maamuma husimama pamoja naye na imamu hubeba Tashahhud hiyo kwa niaba yao, kisha anafanya sujuud ya kusahau mwisho wa swalah.
Baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa imamu hubeba pia kisomo cha al-Faatihah kwa niaba ya maamuma. Kwa mujibu wa wengi ambao wanasema haimlazimu maamuma kuisoma. Lakini kilicho sahihi zaidi ni kwamba maamuma wanawajibika kuisoma na kwamba imamu haibebi kwa niaba yao. Huu ndio msimamo uliochaguliwa kutokana na dalili zenye kuenea. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna swalah kwa yule ambaye hasomi Suurah al-Faatihah.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Katika riwaya nyingine Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliuliza: “Huenda mnasoma nyuma ya imamu?” Tukasema: ”Ndiyo.” Akasema: “Msiwe mnasoma isipokuwa Suurah al-Faatihah, kwani hakuna swalah kwa yule ambaye haisomi.”
Kuna Hadiyth nyingine zinazoonyesha hivyo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1035/ما-يتحمله-الامام-عن-المامومين
- Imechapishwa: 19/01/2026
Swali: Inasemwa kwamba imamu hubeba baadhi ya wajibu kwa niaba ya maamuma. Tunaomba ufafanuzi wa hilo na bayana ya mambo anayobeba.
Jibu: Ndiyo, imamu hubeba baadhi ya mambo kwa niaba ya maamuma. Miongoni mwa hayo ni kwamba yeye hubeba jukumu la sijda ya kusahau kwa niaba yao. Ikiwa maamuma atasahau, basi yeye habebeshwi kitu. Bali imamu ndiye atasujudu nao maamuma husujudu pamoja naye. Ama sahau ya maamuma peke yake wakati yuko nyuma ya imamu, haiwezi kumdhuru. Hairuhusiwi kwake kufanya sujuud ya kusahau peke yake ikiwa ameanza swalah pamoja na imamu tangu mwanzo. Katika hali hiyo imamu hubeba hilo kwa niaba yao. Mfano ni pale imamu anapoacha Tashahhud ya kwanza kwa kusahau na kusimama, basi maamuma husimama pamoja naye na imamu hubeba Tashahhud hiyo kwa niaba yao, kisha anafanya sujuud ya kusahau mwisho wa swalah.
Baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa imamu hubeba pia kisomo cha al-Faatihah kwa niaba ya maamuma. Kwa mujibu wa wengi ambao wanasema haimlazimu maamuma kuisoma. Lakini kilicho sahihi zaidi ni kwamba maamuma wanawajibika kuisoma na kwamba imamu haibebi kwa niaba yao. Huu ndio msimamo uliochaguliwa kutokana na dalili zenye kuenea. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna swalah kwa yule ambaye hasomi Suurah al-Faatihah.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Katika riwaya nyingine Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliuliza: “Huenda mnasoma nyuma ya imamu?” Tukasema: ”Ndiyo.” Akasema: “Msiwe mnasoma isipokuwa Suurah al-Faatihah, kwani hakuna swalah kwa yule ambaye haisomi.”
Kuna Hadiyth nyingine zinazoonyesha hivyo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1035/ما-يتحمله-الامام-عن-المامومين
Imechapishwa: 19/01/2026
https://firqatunnajia.com/majukumu-ya-maamuma-yanabebwa-na-imamu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket