Swali: Ni yepi maoni yenu kuhusu majirani kutembeleana na kukutana kila mmoja akiwa na mke wake, hata kama mwanamke amevaa vazi la kusitiri? Kwa maana kila mmoja anamchukua mke wake na kwenda kwa jirani au rafiki yake na wanakaa pamoja na wanaongea pamoja na kadhalika. Je, hilo ni jambo zuri?

Jibu: Ikiwa wanawake wako pamoja na wanawake, na wanaume wako pamoja na wanaume, na hakuna wanawake kujidhihirisha mbele ya wanaume, kuonyesha mapambo wala kuacha Hijaab, hapana ubaya.

Mwanafunzi: Hapana, wanakaa pamoja.

Ibn Baaz: Ama kukaa wote pamoja bila Hijaab na bila kujali mipaka, basi hili halijuzu. Bali ikiwa wanawake wanakaa na wanawake kwa muda usio wa kukesha, usio wa kupoteza muda na hawakusanyiki juu ya mambo ya batili, hapana ubaya. Wanawake kutembeleana na majirani kutembeleana, hili ni jambo jema baina ya majirani. Kwa sharti kwamba isiwe kwa uovu wala kwa matendo maovu. Isiwe ndani yake mwanamke kujifunua kwa jirani au kwa mume wa jirani au mfano wa hivyo. Hapana. Bali kuwe na haya, sitara na Hijaab. Aidha wanawake wawe na wanawake, na wanaume wawe na wanaume, pais na maasi. Bali matembezi haya kuwepo kheri ndani ya mipaka inayofaa na kwa kukutana kunakofaa kwa kupumzisha nafsi na kuiburudisha na kwa mazungumzo ya kawaida baina ya majirani. Hili halina tatizo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1268/حكم-جلوس-الرجال-والنساء-في-مجلس-واحد-للتحدث
  • Imechapishwa: 15/02/2026