Majimaji yanayotoka wakati wanandoa wanapocheza na kukumbatiana

Swali: Hakuna haya katika dini. Kati yangu mimi na mke wangu kunakuwa kuna michezo na kukumbatiana. Wakati wa kucheza huhisi ladha na baada ya muda huona majimaji yanayonitoka. Je, majimaji haya yanawajibisha mtu kuoga? Je, majimaji haya ni manii? Je, mwanamke anashusha kama anavyoshusha mwanamume kwa namna na rangi? Ni ipi hukumu ya swalah na swawm yangu zilizopita?

Jibu: Kuhusu yale yaliyotajwa na muulizaji kwamba baada ya kutekeleza matamanio yake anatokwa na vitu hivi, hayo ni madhiy na hayawajibishi kuoga. Kwa sababu manii yanayowajibisha kuoga hutoka kwa kasi na kwa ladha tofauti na alivyosema muulizaji ambapo hayakumtoka kwa kasi. Kwa hivyo hayawajibishi kuoga. Kinachomlazimu ni yeye kuosha dhakari yake kisha atawadhe kwa ajili ya swalah.

Kuhusu swali lake kuhusu mwanamke maji yake yanatofautiana na maji ya mwanaume. Maji yake ni mepesi na hayatoki kwa kasi tofauti na maji ya mwanaume. Vilevile maji ya mwanaume yana harufu ambayo inataka kufanana na harufu ya matawi ya mtende tofauti na mwanamke. Maji yake hayana harufu.

Kuhusu yale aliyotaja kwamba aliswali hapo kabla bila kuoga, tunasema kumwambia kwamba kitu hichi hakiwajibishi kuoga. Kinacholazimu ni yeye kuosha tupu ya mwanaume na ya mwanamke. Ikiwa alikuwa hajui jambo hili hana juu yake kitu.

Ama kusema kwamba hakuna haya katika dini, bora angesema kwamba Allaah haoni haya kwa haki. Hivi ndivyo alivyosema Umm Sulaym (Radhiya Allaahu ´anhaa):

“Ee Mtume wa Allaah! Hakika Allaah haoni haya juu ya haki. Je, ni lazima kwa mwanamke kuoga anapoota?”

Ama kusema kwamba hakuna haya katika dini, hili linamfanya mtu kuelewa maana isiyokuwa ya sawa. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Haya ni katika imani.”

Kwa hivyo kuwa na haya katika dini ni katika imani. Lakini wale wanaosema kuwa katika dini hakuna haya wanakusudia kwamba hakuna haya katika mambo ya dini kwa njia ya mtu kuuliza kitu kinachotia haya. Kunasemwa ikiwa haya ndio makusudio basi bora ni kusema kwamba Allaah hastahiki juu ya haki.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/841
  • Imechapishwa: 04/08/2018