Maji yenye kuchanganyika na sabuni  

Swali: Maji yakichanganyika na sabuni yanazingatiwa kuwa ni masafi yanayoweza kusafisha nguo?

Jibu: Ndio, hakuna neno. Sabuni ni safi. Haiathiri. Iko kwa ajili ya usafi. Ni kama mfano wa mkunazi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha maiti aoshwe kwa maji na mkunazi. Sabuni haidhuru. Maji yakichanganyika na sabuni hayadhuriki.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdh–14340204.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020