Swali: Je, wafu walioko makaburini wanahisi wale wanaowasalimia na kuwatembelea?

Jibu: Allaah ndiye anayejua zaidi. Baadhi ya wanazuoni wametaja kuwa wafu wanahisi jambo hilo na hupata faraja kutokana nalo. Lakini mimi sijapata na wala sijui dalili yoyote ya Kishari´ah kutoka katika Sunnah inayofahamisha jambo hilo. Kwa hiyo Allaah ndiye anayejua zaidi. Jambo liliwekwa katika Shari´ah kwetu ni kuwatembelea, kuwaombea dua kwenye makaburi, nyumbani na mahali popote pale. Tuwaombee rehema waislamu waliokufa, kwani hilo linawanufaisha. Vivyo hivyo kutoa swadaqah kwa niaba yao kunawanufaisha. Lakini kuhusu wao kuhisi au kujua anayewatembelea, Allaah ndiye Mwenye kujua. Mimi sijui dalili yoyote iliyo wazi inayojulisha jambo hilo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1160/هل-يشعر-الموتى-بمن-يزورونهم
  • Imechapishwa: 01/02/2026