Mahusiano kati ya mchumba na mchumbiwaji

Swali: Ni upi mpaka wa mahusiano kati ya yule mchumba (خاطب) na mchumbiwaji (مخطوبة)? Je, inafaa kwake kuwa naye faragha na kwenda nae?

Jibu: Hapana, haijuzu. Isipokuwa ikiwa kama atafunga naye ndoa. Hatakiwi kuwa naye faragha. Akitaka kutazama yale yatayomvutia kwa ajili ya kumposa; basi hayo yanatakiwa kufanywa mbele ya walii wake. Haifai kwake kuwa naye faragha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (83) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-15-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 10/02/2018