Mahujaji walioswali kwa kukamilisha Minaa

Swali: Mtu ameswali swalah ya ´Ishaa Rak´ah nne siku ya Tarwiyah huko Minaa. Je, kuna jambo lolote juu yake? Je, yule aliyeswali nyuma yake kama maamuma anatakiwa kumtanabahisha kuhusu hilo?

Jibu: Hakuna jambo juu yake. Lakini lililo sahihi kwa mahujaji ni kuswali Rak´ah mbili. Na Yule anayeswali Rak´ah nne hakuna neno juu yake. Hata hivyo amekwenda kinyume na Sunnah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/199)
  • Imechapishwa: 12/03/2026