Swali: Baadhi ya vijana wanaoshikamana na dini zao wamekuwa wakipambana hata ndani ya nyumba za wazazi wao, kwa sababu wao wanapinga maovu yaliyoingia majumbani na kuharibu nyoyo za watu. Tunaomba muongozo wenu.
Jibu: Anapaswa kuwa na subira. Vijana na wasiokuwa vijana wote wanapaswa kuwa na subira. Ikishaingia mitihani ndani ya nyumba, basi anapaswa kuwa na subira. Huu ni wakati wa subira. Ni wakati wa fitina na mitihani. Basi awe na subira, ajitahidi kadiri ya uwezo wake na amuombe Allaah msaada katika hilo. Akifaulu kujitenga na kuishi peke yake ikiwa hawamkubalii na hawamtii katika kuondoa maovu, basi hapana tatizo ajitenge kama anaweza kuishi katika nyumba yake. Asipoweza, basi ajitahidi na amche Allaah. Allaah hamkalifishi mtu isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake. Asihudhurie maovu.
Daraja za kukemea maovu ni tatu:
1 – Kwa mkono.
2 – Kwa ulimi.
3 – Kwa moyo.
Ya kwanza ni kwa mkono ikiwa anaweza. Ikiwa yeye ndiye mkuu wa nyumba au anayeweza kufanya atakavyo. Ikiwa si mkuu wa nyumba, bali yuko pamoja na wazazi wake na kaka zake wakubwa, basi akemee kadiri awezavyo kwa ulimi. Wasipokubali, basi akemee kwa moyo wake. Akifaulu kujitenga na kuishi peke yake, basi afanye hivyo. Hii ndiyo jitihada ya maisha haya. Maisha ya jitihada. Lazima kuwe na subira na lazima kuwe na jitihada kadiri ya uwezo:
”fataqu…tum”
Swali: Je, hili linahesabiwa kuwa katika kupambana Jihaad?
Jibu: Bila shaka. Kukemea maovu ni katika ulinganizi na kupambana Jihaad.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/975/الحث-على-الصبر-في-الدعوة-الى-الله
- Imechapishwa: 23/12/2025
Swali: Baadhi ya vijana wanaoshikamana na dini zao wamekuwa wakipambana hata ndani ya nyumba za wazazi wao, kwa sababu wao wanapinga maovu yaliyoingia majumbani na kuharibu nyoyo za watu. Tunaomba muongozo wenu.
Jibu: Anapaswa kuwa na subira. Vijana na wasiokuwa vijana wote wanapaswa kuwa na subira. Ikishaingia mitihani ndani ya nyumba, basi anapaswa kuwa na subira. Huu ni wakati wa subira. Ni wakati wa fitina na mitihani. Basi awe na subira, ajitahidi kadiri ya uwezo wake na amuombe Allaah msaada katika hilo. Akifaulu kujitenga na kuishi peke yake ikiwa hawamkubalii na hawamtii katika kuondoa maovu, basi hapana tatizo ajitenge kama anaweza kuishi katika nyumba yake. Asipoweza, basi ajitahidi na amche Allaah. Allaah hamkalifishi mtu isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake. Asihudhurie maovu.
Daraja za kukemea maovu ni tatu:
1 – Kwa mkono.
2 – Kwa ulimi.
3 – Kwa moyo.
Ya kwanza ni kwa mkono ikiwa anaweza. Ikiwa yeye ndiye mkuu wa nyumba au anayeweza kufanya atakavyo. Ikiwa si mkuu wa nyumba, bali yuko pamoja na wazazi wake na kaka zake wakubwa, basi akemee kadiri awezavyo kwa ulimi. Wasipokubali, basi akemee kwa moyo wake. Akifaulu kujitenga na kuishi peke yake, basi afanye hivyo. Hii ndiyo jitihada ya maisha haya. Maisha ya jitihada. Lazima kuwe na subira na lazima kuwe na jitihada kadiri ya uwezo:
”fataqu…tum”
Swali: Je, hili linahesabiwa kuwa katika kupambana Jihaad?
Jibu: Bila shaka. Kukemea maovu ni katika ulinganizi na kupambana Jihaad.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/975/الحث-على-الصبر-في-الدعوة-الى-الله
Imechapishwa: 23/12/2025
https://firqatunnajia.com/mahimizo-ya-kuwa-na-subira-katika-kulingania-kwa-allaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket