Mahimizo ya kukhafifisha swalah na wakati huohuo kuikamilisha

Swali: Ni vipi tutaoanisha kati ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Je, ni mfitini wewe, ee Mu´aadh?”

na kitendo chake yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa vile imethibiti ya kwamba alisoma al-Baqarah, Aal ´Imraan, al-Maaidah, al-A´raaf na nyenginezo?

Jibu: Makusudio yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kuhimiza kukhafifisha pindi mtu anapokuwa imamu anayewaswalisha watu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote katika nyinyi atakayeswalisha watu basi akhafifishe. Hakika katika wao yupo mdogo, mtumzima, mnyonge na mwenye haja. Akiswali peke yake basi arefushe anavotaka.”[1]

Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mtu mwenye kukhafifisha swalah zaidi katika ukamilifu wake. Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Nimeswali nyuma ya mtu anayekamilisha swalah. Wala hakuna yeyote anayekhafifisha swalah kama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[2]

Kuna maafikiano juu yake.

Lakini akiswali peke yake arefushe anavotaka.

Kisomo chake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) cha al-Baqarah, an-Nisaa´ na Aal ´Imraan ilikuwa ni katika swalah ya usiku.

[1] al-Bukhaariy (662) na Muslim (714).

[2] al-Bukhaariy (667) na Muslim (721).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/90)
  • Imechapishwa: 21/11/2021