Magonjwa ya sehemu za siri kabla ya Qiyaamah

Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Hebu nikuelezeni niliyosikia kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambayo hakuna yeyote aliyasikia kutoka kwake ambaye atakusimulieni nayo baada yangu? Miongoni mwa alama za Saa ni kunyanyuliwa elimu, kuenea kwa ujinga na kudhihiri kwa uzinzi.”[1]

Kwa sababu ya kuenea kwa uzinifu waislamu wamepatwa na maradhi ambayo hayakuwepo kwa babu zao. ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kamwe hayatoenea machafu kwa watu mpaka wakayatangaza hadharani, isipokuwa watapewa mtihani wa tauni na maradhi ambayo hayakuwa kwa babu zao.”[2]

Wakati wamarekani walipojiingiza katika mambo ya uzinzi na hakuna mamlaka ya kidini iliyowazuia, ndipo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) akawajaribu kwa magonjwa kama vile kisonono na kaswende ambayo yaliwaweka madaktari katika mtihani kwa muda mrefu. Kisha baada ya hapo Allaah (Subhaanah) akawajaribu kwa ukimwi ambao mamilioni ya watu wanaweza kuwa wameambukizwa. Wakawa ni wenye kufadhaika na wenye kuogopa sana kwa sababu ya ukimwi ambao mpaka sasa madaktari bado hawajaweza kupata tiba.

[1] Muslim (2671).

[2] Ibn Maajah (4019), at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Awsatw” (4671) na al-Haakim (8623). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy´” (7978).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 243
  • Imechapishwa: 31/03/2025