Maghrib moja kwa moja baada ya adhaana

Swali: Inafaa kuswali Maghrib baada tu ya adhaana au mtu acheleweshe dakika kumi?

Jibu: Muadhini akishaadhini basi umeingia wakati wa swalah. Mtu anaweza kuswali moja kwa moja baada ya adhaana. Kwa sababu wakati wa swalah umeshaingia.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/فتاوى-على-الهواء-13-11-1435هـ-0
  • Imechapishwa: 19/06/2022

Turn on/off menu