Maelezo ya Ibn-ul-Qayyim na kazi ya al-Arna´uut katika “at-Twibb an-Nabawiy”

Swali: Katika “at-Twibb an-Nabawiy” Ibn-ul-Qayyim ametaja Hadiyth nyingi bila ya kuzitajia hukumu yake. Unasamaje kama unaziwekea taaliki?

Jibu: Udhahiri ni kwamba Shu´ayb al-Arna´uut ameziwekea taaliki, ingawa hakuzipa haki yake. Baadhi ya ndugu wameazimia kuandika kitabu ambapo wanataja tu zile Hadiyth ambazo ni Swahiyh. Ni jambo zuri. Kwa hali yoyote, kuna maelezo kadhaa katika kitabu cha Ibn-ul-Qayyim ambayo hayafai kutumiwa. Ni lazima kuyakagua na kuyatazama vyema.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 421
  • Imechapishwa: 14/07/2025