Madhehebu manane kuhusiana na maneno ya Allaah

Watu wamelumbana juu ya maneno ya Allaah na wako katika madhehebu mbali mbali. Lakini madhehebu muhimu katika mambo haya ni manane. Haya ni madhehebu ya watu wote walioko katika ardhi. Madhehebu yote masaba ni ya batili. Na dhehebu moja ndio lenye haki. Pamoja na kwamba madhehebu haya masaba ni batili, ´Allaamah Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) anasema yamezidi kuwa mengi kati ya watu ulimwenguni na hawajui mengine pamoja na ubatili wake. Katika madhehebu haya saba kuna ambayo ni ya kufuru ya mengine ni ya Bid´ah.

1- Madhehebu ya kwanza ni Ittihaadiyyah.

2- Madhehebu ya pili ni Falaasifah.

3- Madhehebu ya tatu ni Saalimiyyah.

4- Madhehebu ya nne ni Karraamiyyah.

5- Madhehebu ya tano ni Kullaabiyyah.

6- Madhehebu ya sita ni Ash´ariyyah.

7- Madhehebu ya saba ni Jahmiyyah na Mu´tazilah.

8- Madhehebu ya nane ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

Haya ndio madhehebu muhimu ya watu walioko ardhini kuhusiana na ni nini maneno ya Allaah. Kuna madhehebu mengine lakini hata hivyo hayajulikani.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/154-155)
  • Imechapishwa: 31/05/2020