Madhambi ambayo muislamu amekufa kabla ya kutubia kwayo

Swali: Vipi kuhusu madhambi ambayo mtu amekufa juu yake na hakutubia kwayo?

Jibu: Hukumu ni hiyohiyo kama ilivyokuja katika Hadiyth. Alipomsitiri duniani baina Yake na yeye atamsamehe (Subhaanahu wa Ta´ala). Pengine yakawa ni miongoni mwa yale madhambi madogo ambayo yanasamehewa kwa kujiepusha na madhambi madogo:

إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ

“Mkijiepusha madhambi makubwa mnayokatazwa Tutakufutieni madhambi yenu.”[1]

Mja anajiepusha na madhambi madogo na hivyo anasamehewa madhambi madogo. Huenda makosa hayo ameyafanya baina ya mja na Mola wake na hakuna ayajuaye isipokuwa tu Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) na mja hakuweza kutubia kwayo. Matokeo yake Allaah akamsamehe kwayo kutokana na mema na matendo yake mazuri ambayo ni mengi na Allaah kumridhia. Yale mema aliyoyafanya yanakuwa ni kama tone la maji baharini. Tone la uchafu kwenye bahari ya mambo ya kheri na hivyo Akamsamehe (Subhaanahu wa Ta´ala) kwayo.

[1] 04:31

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24472/حكم-ذنوب-المسلم-التي-مات-ولم-يتب-منها
  • Imechapishwa: 23/10/2024