Madeni ya kafiri baada ya kusilimu

Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye alikuwa kafiri kisha akasilimu, naye alikuwa mfanyabiashara na akaacha madeni?

Jibu: Akisilimu, anapaswa kulipa deni alilonalo. Ni lazima. Analipa deni ikiwa wadai wake watamtaka kulilipa. Endapo watamsamehe, Allaah awalipe kheri.

Swali: Hata ikiwa madeni hayo yalikuwa katika biashara ya pombe?

Jibu: Hapana, hapana. Inahusiana na madeni yanayokubalika kwa mujibu wa Shari´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25400/حكم-من-كان-كافرا-ثم-اسلم-وعليه-ديون-للناس
  • Imechapishwa: 09/03/2025