Swali: Ni ipi hukumu ya kutengeneza nywele kwa wanaume na wanawake? Je, ni jambo linalomhusu mwanaume pekee au wote?
Jibu: Kanuni ni kuwa yale yanayokuja katika amri na makatazo yanawahusu wote, wanaume na wanawake, isipokuwa ikipatikana dalili maalum ya kubainisha kuwa jambo fulani ni la kundi maalum tu. Kutengeneza nywele baadhi ni jambo lenye manufaa zaidi, kwa sababu kufanya hivyo kila siku kunaweza kuleta mashaka na kupetuka mipaka ya anasa. Lakini imekuja katika Hadiyth kwamba Mtume alimpa ruhusa Abu Qataadah alipolalamika kuwa anahitaji kufanya hivyo kila siku. Kwa hiyo inaonekana – na Allaah ndiye anajua zaidi – ni kwamba makatazo yaliyokuja ni ya kuchukiza. Lakini ikitokea haja ya kutengeneza nywele kwa sababu ya jambo maalum, basi hakuna tabu kufanya hivyo kila siku. Kutengeneza nywele ni kuzifungua, kuzichana na kuzitunza.
Swali: Ikiwa mwanaume anataka mke wake afanye hivyo kila siku ili apendeze kwake kutokana na nywele zake?
Jibu: Sunnah ni kufanya hivyo baada ya muda fulani fulani, kama alivyoeleza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hiyo ndiyo sunnah.
Swali: Hadiyth zote katika jambo hili ni Swahiyh?
Jibu: Ninavyojua ni kuwa zote ni Swahiyh. Hadiyth ya ´Abdullaah bin Mughaffal ina kupokezana kutoka kwa al-Hasan. Hata hivyo inaonekana kuwa imekuja kupitia njia nyingine zisizo za an-Nasaa’iy. Hadiyth ya Abu Qataadah nayo haina tabu. Ama hapa kupitia njia ya al-Hasan kuna Swahabah anayekosekana katika cheni ya wapokezi na ina kupokezana.
Swali: Ina maana kwamba wakati wa haja machukizo yanaondoka?
Jibu: Ndivyo inavyoonekana – na Allaah ndiye anajua zaidi – ikipatikana haja kutokana na dalili ya Hadiyth ya Abu Qataadah.
Swali:
”Yule mwenye nywele basi azitunze.”?
Jibu: Kwa njia ya iliyowekwa katika Shari´ah; azitunze kwa njia ya Kishari´ah.
Swali: Hadiyth hiyo ni Swahiyh?
Jibu: Sijui hali yake.
Swali: Je, kutengeneza ndevu kunalinganishwa na kutengeneza nywele za kichwani?
Jibu: Haionekani hivyo. Ndevu haziguswi.
Swali: Wanaosema kutengeneza ni kwa nywele za kichwa tu?
Jibu: Hilo ndilo linalojulikana. Kutengeneza ni kwa nywele za kichwa.
Swali: Basi ndevu hazihusiki?
Jibu: Hapana, hazihesabiwi kama kutengeneza.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31629/ما-حكم-ترجيل-الشعر-للرجال-والنساء
- Imechapishwa: 12/12/2025

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31629/ما-حكم-ترجيل-الشعر-للرجال-والنساء
Imechapishwa: 12/12/2025
https://firqatunnajia.com/machukizo-ya-kutengeneza-na-kuchana-nywele-kila-siku/