Swali: Ipi hukumu ya maandamano ikiwa yataungwa mkono na mtawala… ?

Jibu: Hapana! Maandamano hayajuzu, sawa yakiungwa mkono au hapana. Maandamano ni fujo na yanachangia madhara mengi. Na Uislamu ni dini ya kimya na ya uthabiti. Hakuna maandamano katika Uislamu.

Mtawala hakuamrisha hilo na hata akiamrisha hili atanasihiwa [kwamba halifai]. Ataambiwa kuwa hili si katika maslahi ya waislamu bali ni mpango wa makafiri.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.youtube.com/watch?v=HFRmUJOtOnU
  • Imechapishwa: 05/09/2020