Swali: Swawm ya mwaka mzima (صيام الدهر) ni nini? Je, inajuzu kufunga masiku mfululizo kwa mujibu wa Hadiyth yenye maana kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwauliza watu wake kuhusu chakula na asipopata basi alikuwa ananuia kufunga? Je, inajuzu kwangu kufunga kwa sababu ya hali ngumu ya kifedha?
Jibu: Hakuna tatizo juu ya funga ya kujitolea. Mtu akitaka anaweza kuanza kufunga katikati ya mchana ikiwa hajala kabla yake, basi anaweza kufunga kutoka katikati ya mchana. Hakuna shida. Vilevile ambaye anafunga swawm ya kujitolea akitaka anaweza pia kufungua.
Lakini kufunga mfululizo kunapaswa kuwa kwa mtindo wa siku moja kufunga na siku moja kula. Ikiwa mtu anataka kufunga mfululizo, basi afunge siku moja na afungue siku moja. Na hapana vibaya ikiwa atafunga siku nyingi mfululizo kisha akafungua kwa idadi hiyohiyo ya siku, kama alivyokuwa akifanya ´Abdullaah bin ´Amr mwishoni mwa maisha yake. Alipokuwa akihisi uchovu, alikuwa akifunga siku nyingi mfululizo, kisha akifungua kwa idadi hiyohiyo ya siku, kwa sababu ilikuwa rahisi zaidi kwake.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25436/ما-معنى-صوم-الدهر-وحكم-الصوم-لظروف-المعيشة
- Imechapishwa: 20/03/2025
Swali: Swawm ya mwaka mzima (صيام الدهر) ni nini? Je, inajuzu kufunga masiku mfululizo kwa mujibu wa Hadiyth yenye maana kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwauliza watu wake kuhusu chakula na asipopata basi alikuwa ananuia kufunga? Je, inajuzu kwangu kufunga kwa sababu ya hali ngumu ya kifedha?
Jibu: Hakuna tatizo juu ya funga ya kujitolea. Mtu akitaka anaweza kuanza kufunga katikati ya mchana ikiwa hajala kabla yake, basi anaweza kufunga kutoka katikati ya mchana. Hakuna shida. Vilevile ambaye anafunga swawm ya kujitolea akitaka anaweza pia kufungua.
Lakini kufunga mfululizo kunapaswa kuwa kwa mtindo wa siku moja kufunga na siku moja kula. Ikiwa mtu anataka kufunga mfululizo, basi afunge siku moja na afungue siku moja. Na hapana vibaya ikiwa atafunga siku nyingi mfululizo kisha akafungua kwa idadi hiyohiyo ya siku, kama alivyokuwa akifanya ´Abdullaah bin ´Amr mwishoni mwa maisha yake. Alipokuwa akihisi uchovu, alikuwa akifunga siku nyingi mfululizo, kisha akifungua kwa idadi hiyohiyo ya siku, kwa sababu ilikuwa rahisi zaidi kwake.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25436/ما-معنى-صوم-الدهر-وحكم-الصوم-لظروف-المعيشة
Imechapishwa: 20/03/2025
https://firqatunnajia.com/maana-ya-swawm-ya-mwaka-mzima-na-mtu-kufunga-kwa-sababu-ya-hali-ngumu-ya-kifedha/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket