Swali: Majina ya Allaah na sifa Zake ni katika aina ya Aayah zilizo wazi na si katika aina ya Aayah zisizo wazi au ni kwamba kwa upande wa maana ziko wazi na kwa upande wa jinsi ni katika Aayah zisizo wazi?
Jibu: Ni katika Aayah zilizo wazi. Majina mazuri ya Allaah ni katika Aayah zilizo wazi kwa upande wa maana, lakini inapokuja katika namna haijulikani isipokuwa na Allaah pekee. Kwa ajili hii Salaf (Radhiya Allaahu ´anhum) wamesema kuhusu sifa kwamba maana yake inajulikana, namna yake haijulikani. Kulingana juu ni jambo linalojulikana, rehema inajulikana, ghadhabu inajulikana, radhi inajulikana na kuchuka kunajulikana. Lakini namna yake haijulikani, namna yake haijulikani kabisa.
Kwa hiyo Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaamini majina na sifa, kwamba ni haki na kwamba maana yake yanajulikana. Hata hivyo namna yake haijulikani isipokuwa na Allaah. Kwa ajili hiyo Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) amesema:
”Kulingana juu kunajulikana. Namna haijulikani.”
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30979/هل-اسماء-الله-وصفاته-من-المحكم-ام-المتشابه
- Imechapishwa: 19/09/2025
Swali: Majina ya Allaah na sifa Zake ni katika aina ya Aayah zilizo wazi na si katika aina ya Aayah zisizo wazi au ni kwamba kwa upande wa maana ziko wazi na kwa upande wa jinsi ni katika Aayah zisizo wazi?
Jibu: Ni katika Aayah zilizo wazi. Majina mazuri ya Allaah ni katika Aayah zilizo wazi kwa upande wa maana, lakini inapokuja katika namna haijulikani isipokuwa na Allaah pekee. Kwa ajili hii Salaf (Radhiya Allaahu ´anhum) wamesema kuhusu sifa kwamba maana yake inajulikana, namna yake haijulikani. Kulingana juu ni jambo linalojulikana, rehema inajulikana, ghadhabu inajulikana, radhi inajulikana na kuchuka kunajulikana. Lakini namna yake haijulikani, namna yake haijulikani kabisa.
Kwa hiyo Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaamini majina na sifa, kwamba ni haki na kwamba maana yake yanajulikana. Hata hivyo namna yake haijulikani isipokuwa na Allaah. Kwa ajili hiyo Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) amesema:
”Kulingana juu kunajulikana. Namna haijulikani.”
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30979/هل-اسماء-الله-وصفاته-من-المحكم-ام-المتشابه
Imechapishwa: 19/09/2025
https://firqatunnajia.com/maana-ya-sifa-na-majina-ya-allaah-inatambulika-namna-haitambuliki/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket