Maana ya mwanamke kukaa eda

Eda ya kujizuia ni kuacha mapambo, manukato, vipodozi na mfano wa hayo katika muda wa kukaa eda mpaka eda iishe. Wafikishiwe hili. Ni wajibu wafikishiwe kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alieamrisha kukaa eda mwanamke kwa ajili ya mume kuwa miezi minne na siku kumi. Eda ya kujizuia ni kuacha kila kinachowafanya watu wamvutie au amtamani kwa aina za uzuri kama nguo nzuri, manukato, pambo, wanja na yanayofanana na hayo. Anatakiwa akae nyumbani kwake katika muda wa eda mpaka eda ya kifo iishe. Akiwa ni mjamzito eda yake inaisha kwa kujifungua.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1252/هل-يجوز-للمراة-ترك-الاحداد-على-زوجها
  • Imechapishwa: 14/02/2026