Maana ya maneno ya ´Umar kuita Tarawiyh kuwa ni Bid´ah

Swali: Kuhusiana na Bid´ah baadhi ya watu wanatumia kama dalili maneno ya ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) wakati alipowakusanya Maswahabah katika swalah ya Tarawiyh na akasema:

”Neema ya Bid´ah!”

Ahl-ul-Bid´ah wanajengea hii kama hoja.

Jibu: Hii ni kwa upande wa lugha. Vinginevyo ni Sunnah iliyofanywa na Mtume (Swala Allaahu ´alayhi wa sallam), akaiweka katika Shari´ah na akalingania kwayo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikufa bila kuwakusanya nyuma ya imamu mmoja na hilo likaja kuhuishwa na ´Umar na akawakusanya. Inaitwa kuwa ni Bid´ah upande wa lugha na si kwa upande wa Shari´ah.

Swali: Mwenye kujengea hoja hii hoja yake ni batili?

Jibu: Hata tukikadiria kuwa ´Umar amesema hivo ´Umar hakukingwa na kukosea. ´Umar ni mmoja katika Maswahabah. Yeye sio hoja. Hoja ni katika maneno ya Allaah na Mtume Wake. Lakini maneno yake yanatakiwa kufasiriwa vizuri ili mtu asimjengee dhana mbaya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21527/ما-معنى-قول-عمر-نعمت-البدعة
  • Imechapishwa: 23/08/2022