Maana ya kuharibika matendo kwa mwenye kuacha ´Aswr

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kuacha swalah ya ´Aswr basi yameporomoka matendo yake.”

Inafahamisha nini?

Jibu: Ukafiri wa mwenye kufanya hivo. Ni kama mfano wa yale yaliyopokelewa katika Hadiyth nyingine:

“Baina ya mtu na shirki na ukafiri na shirki ni kuacha swalah.”

“Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yule atakayeiacha amekufuru.”

Ukafiri unaporomosha matendo. Tunamuomba Allaah afya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21633/معنى-حبوط-العمل-لمن-ترك-صلاة-العصر
  • Imechapishwa: 01/09/2022