Swali: Je, inasemwa kwamba Allaah yuko (في) mbinguni au juu ya mbingu?

Jibu: Alipoulizwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah yuko wapi?” Akajibu: “Yuko mbinguni.”

Kwa maana yuko juu ya mbingu baada ya kuulizwa na mjakazi. Neno mbingu hapa linamaanisha juu. Kama Allaah alivyosema (Ta´ala):

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ

“Je, mnadhani mko katika amani na aliyeko juu mbinguni?”[1]

Kwa maana Aliye juu. Kwa sababu neno “mbingu” (السماء) hutumika kwa maana mbili:

1 – Hutumika kumaanisha mbingu iliyojengwa.

2 – Pia hutumika kumaanisha ujuu.

[1] 67:16

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31658/هل-يقال-الله-في-السماء-او-فوق-السماء
  • Imechapishwa: 14/11/2025