Maamuma wanaojichelewesha kwa sababu imamu hafanyi Qunuut

Swali: Baadhi ya watu wanaofuata kibubusa wakiswali nyuma ya anayeswali bila Qunuut, huchelewa na kufanya Qunuut wao binafsi na kumuacha imamu akisujudu.

Jibu: Hapana, haifai kufanya hivyo. Imamu amewekwa ili afuatwe, basi msikhitilafiane naye. Akiwa ameswali nyuma ya asiyekunuti, afanye kama yeye. Asujudu naye na aache Qunuut, kwa kuwa Qunuut haina asili ya kudumu. Bali huwa katika hali za dharurah. Mtume hakuwa akiendelea nayo daima.

Swali: Vipi ikiwa imamu atafanya Qunuut?

Jibu: Akifanya Qunuut pamoja naye, hakuna tatizo, kwa sababu ana hoja ya madhehebu ya ash-Shaafi´iy na baadhi ya wengine.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31477/ما-حكم-من-تاخرعن-الامام-ليقنت-لنفسه
  • Imechapishwa: 24/10/2025