Maafikiano ya mapendezo ya kuanza kutoa salamu

Swali 664: Ni nini kinachoondoa wajibu katika kuanzisha salamu kutokana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Ukikutana naye basi mtolee salamu.”?

Jibu: Sijui. Maoni yanayosema kwamba ni wajibu haiko mbali, kwa sababu amri ziko wazi[1].

[1] Ibn  ´Abd-ul-Barr amepokea maafikiano kwamba kuanzisha salamu kwa salamu ni Sunnah. Kwa hiyo mtu atazame kama maafikiano hayo yamesihi au hapana. Kundi la wanazuoni wamepokea maelezo ya Ibn ´Abd-ul-Barr kuhusu maafikiano hayo na hawakuyapinga. Miongoni mwao ni:

1 – an-Nawawiy katika ”Sharh Muslim” (14/104).

2 – Haafidhw katika ”al-Fath” (11/4).

3 – al-Munaawiy katika ”Faydhw-ul-Qadiyr” (1/305).

4 – ash-Shawkaaniy katika ”Nayl-ul-Awtwaar” (4/44).

5 – al-Mubaarakfuuriy katika ”Tuhfat-ul-Ahwadhiy” (7/390).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 241
  • Imechapishwa: 26/06/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´