Lini mtu anahesabiwa kuwahi swalah ya mkusanyiko? II

Swali: Je, anayefika akamkuta imamu yuko katika Tashahudi ya mwisho katika swalah yake huhesabiwa kuwa amewahi swalah ya mkusanyiko?

Jibu: Ikiwa alichelewa kwa udhuru, basi ana ujira wa swalah ya mkusanyiko, hata kama hakuwahi swalah yenyewe. Kwa maana nyingine akichelewa kwa udhuru unaokubalika katika Shari´ah, kwa maana alikusudia kuswali lakini kukawa na kizuizi kilichomzuia, kama vile kukidhi haja kubwa au ndogo au mfano wa hilo, basi atapata ujira wa swalah ya mkusanyiko. Lakini kuhusu yule aliyepuuza na hakupata chochote isipokuwa Tashahudi, basi hakuwahi swalah ya mkusanyiko. Swalah ya mkusanyiko haidirikiwi isipokuwa kwa kuwahi angalau Rak´ah moja. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayewahi Rak´ah moja ya swalah, basi amewahi swalah.”

Kwa hiyo sahihi ni kwamba swalah ya mkusanyiko haipatikani isipokuwa kwa kuwahi Rak´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1492/هل-يثبت-فضل-الجماعة-بادراك-التشهد-الاخير
  • Imechapishwa: 21/12/2025