Lau waislamu wangeshikamana na mwongozo wa talaka

Mwanamke haachwi isipokuwa katika hali mbili:

1 – Ndani ya twahara ambayo hakumwingilia ndani yake. Kwa maana nyingine amesafika lakini hakumwingilia; anampa talaka moja na haiongezi juu yake.

2 – Katika hali ya kuwa mjamzito, kama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyomwambia Ibn ´Umar amshike, kisha amtaliki kabla ya kumwingilia katika hali ya twahara au akiwa mjamzito.

Hii ndiyo Sunnah, ima ampe talaka akiwa katika twahara au akiwa mjamzito katika hali hizi mbili. Kisha talaka iwe talaka moja tu na asiiongeze. Hiki ndicho kilichopendekezwa.

Lau waislamu wangelishikamana na jambo hili na wakatembea juu yake, basi kungelikuwepo furaha kwa wote, kheri kwa wote, talaka ingepungua na wanawake wangejenka… Lakini pupa, haraka, kutokujali na kutokuwa na kuangalia mwisho wa mambo kunawaingiza watu katika shari nyingi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/مسالة-الطلاق-ثلاثا-او-واحدة
  • Imechapishwa: 15/02/2026