Lakabu ya mtoto wa kiume, na si mtoto wa kike

Swali: Ikiwa mtoto mkubwa wa mtu ni msichana aitwe lakabu kwa jina lake?

Jibu: Hapana, ni bora mtu aitwe lakabu kwa jina la mtoto wa kiume. Mtu haulizii juu ya wasichana zake. Aitwe lakabu kwa jina la mtoto wa kiume kama vile Abu Shurayh. Hata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) lakabu yake ilikuwa Abul-Qaasim, ingawa Qaasim sio mtoto wake mkubwa.

Swali: Vipi jambo la mtu ambaye Allaah amemjaalia watoto wake wote ni wa kike?

Jibu: Si lazima kuwa na lakabu. Anaweza kujiita lakabu kwa jina jingine. Hata hivyo sitambui kama kuna ubaya kama atataka kujiita lakabu ya Abu Faatwimah au Abu ´Aaishah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24671/هل-يكنى-بالبنت-اذا-كانت-اكبر-الاولاد
  • Imechapishwa: 20/11/2024