Laana kwa mwanamke anayeondoa nyusi

Swali: Namsw (النمص) ni nini? Ni ipi hukumu yake? Hufanyika katika sehemu gani ya mwili wa mtu? Je, inawahusu wanaume na wanawake?

Jibu: Namsw (النمص) ni kung’oa nywele za nyusi. Baadhi ya wanazuoni wameambatanisha pia nywele za kawaida za usoni. Hivyo haijuzu kuzinyoa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani mwanamke anayeng’oa nyusi na yule anayeng’olewa. Wanazuoni wamesema kuwa Namsw (النمص) ni kung’oa nywele za nyusi kwa kutumia kifaa cha kun’goa, yaani koleo. Mwanamke hujipamba kwa nyusi zake kwa kutumia koleo hadi kung’oa baadhi ya nywele. Ikiwa kwa koleo ni haramu, basi vipi kwa njia kali zaidi kuliko koleo?

Swali: Vipi kuhusu nywele za mikono na miguu?

Jibu: Nywele za mikono na miguu hakuna jambo lililopokelewa kuhusu hilo. Hatufahamu chochote kilichothibiti juu yake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1955/حكم-النمص
  • Imechapishwa: 30/05/2026