Swali: Je, anayefanya kazi benki amelaaniwa?

Jibu: Anaingia katika kundi hili; mla ribaa, mtoa riba, mwandishi na shahidi wake, kwani wote ni wasaidizi wa batili. Allaah amesema:

وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

“Wala msishirikiane katika dhambi na uadui.” (05:02)

Hukumu hiyohiyo inawagusa wafanyakazi wengine wa benki.

Swali: Je, hii ni miongoni mwa madhambi makubwa?

Jibu: Ndiyo, ni miongoni mwa madhambi makubwa, kwani madhambi ambayo mtendaji wake amelaaniwa ni katika madhambi makubwa. Tunamuomba Allaah usalama.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31638/من-يعمل-في-البنك-هل-هو-ملعون
  • Imechapishwa: 12/11/2025