11 – Abu Ibraahiym Isma´iyl bin al-´Abbaas amesema:

“Nimemsikia Shaqiyq, mtumwa wa kiume wa al-Answaariy, akiulizwa kuhusu ndoto ya al-Answaariy juu ya ‘Amr bin ´Ubayd. Nikasema: “Ameota nini?” Amesimulia ya kwamba amesema: “Nimemuona akibadilika na kuwa tumbili na mnyororo shingoni mwa mchimba kaburi. Nikasema: “Ee Abu ´Uthmaan! Ni nini kimefanya kuwa hivi?” Akasema: “Maneno yangu juu ya makadirio.” Nikamuuliza al-Answaariy juu ya hilo na akasema: “Ee mwanangu mpendwa! Msitaje makosa ya wanazuoni.”

12 – ´Amr bin Swaalih al-Mukhtaar amesema:

“Nilikuwa kwa Hishaam bin Hassan wakati ´Amr bin ´Ubayd alipotajwa. Nikaona jinsi alivyokasirika. Akasema: Naapa kwa jina la Allaah kwamba hakuna kinachomzidishia mzushi isipokuwa ni kuwa mbali zaidi na Allaah kwa vitendo vyake na hakuna Allaah anachomzidishia isipokuwa kumkasirikia zaidi.”

13 – Ma´mar amesema:

“Ayyuub [as-Sikhtiyaaniy] alikuwa akisema: “Amefanya nini anayechukia ‘Amr bin ‘Ubayd? Sijawahi ‘Amr bin ‘Ubayd hata siku kuwa ni mwenye akili.”

14 – Sufyaan bin Mu´aadh bin Mu´aadh amesema:

“Nilizungumza na ´Amr bin ‘Ubayd juu ya mirathi ya mwanamke aliyetalikiwa kabisa. Nikawa najenga hoja dhidi yake kwa maoni ya ‘Uthman (Radhiya Allaahu ´anh) na kwamba anamruhusu yeye kurithi. Akasema: “Harithi kabisa.” Nikasema: “´Uthmaan ndio hoja yangu.” Akasema: “´Uthmaan hakuwahi kuwa hoja yoyote wala Sunnah.”

15 – ´Amr bin Nadhwr:

“Nilipita karibu na ‘Amr bin ‘Ubayd akiwa amekaa. Nikakaa naye. Akataja kitu na nikasema: “Hivyo hawasemi maswahiba zetu.” Akasema: “Maswahiba zako ni kina nani  umkose baba yako?” Nikasema: ”Ayyuub, Yuunus, Ibn ´Awn na at-Taymiy.” Akasema: “Wao ni wachafu na najisi na wafu. Hawako hai.”

  • Muhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy (afk. 385)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Akhbaar ´Amr bin ´Ubayd bin Baab al-Mu´taziliy, uk. 96-100
  • Imechapishwa: 22/11/2025